News | 02 Mar, 2023

Intergovernmental Standing Committee on Shipping

English

ISCOS brings together stakeholders to discuss the importance of owning ships in transportation

Secretary General Ministry of Construction and Transport Mr. Gabriel Migire has said that at present the business of water transportation in the African continent has been due to many cargoes transported in the world coming from and coming to Africa.
Mr. Migire said this today, February 27, 2023, during the Meeting of the Institute involved in maritime transport issues (ISCOS), held at the Four Points hotel in Dar es Salaam.
“We as Africans have every reason to ensure that we have people who own water transport”.
In addition, he said that there is a challenge of lack of learning tools for the students studying at the Maritime College (DMI) when they finish the seafaring training.
“We need to have our instruments but we also need these instruments to do business because Africa is now being opened for business” said Mr. Migire.
“We in this region of East Africa and ISCOS member states have reason to make sure that we use the opportunity to participate in the African trade. As we open the African countries to each other, it does not mean that we allow other continents to come and do business in Africa, it is us African countries who have to ensure we use that opportunity” added Mr. Migire.
For his part, the Secretary General of ISCOS, Daniel Kiange has said that the time has come for Africa to be able to have transportation facilities to facilitate the transportation of goods abroad.
“Let’s have our own ships that can carry cargo to China, South Africa and elsewhere so that the money can stay in our region, and we can also create jobs for our young people,” said Kiange.
And the Executive Secretary of the African Shipowners Association (African Shipowners Association), Ms. Funmi Folorunso said that following the meeting they expect the ISCOS Member States to come up with a policy on ship ownership to support the shipping industry.
Godwin Isdore from Songoro Marine is one of the stakeholders who participated in the meeting, he said that participating in the meeting is to increase knowledge as well as build relationships with stakeholders from Iscos member countries, including from Kenya and the Democratic Republic of Congo (DRC).
“If we look at Africa, one of the biggest businesses that is taking place is Shipping and as you can see the stakeholders have woken up and are saying that now is the time to own ships” Godwin said.
The Intergovernmental Standing Committee on Shipping (ISCOS) is an institution involved in maritime transport issues which currently includes the countries of TANZANIA, KENYA, UGANDA, ZAMBIA and DRC.
Swahili

ISCOS yakutanisha wadau kujadili umuhimu wa kumiliki Meli katika usafirishaji

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Bw. Gabriel Migire amesema Kwa sasa Biashara ya Usafirishaji kwa njia ya maji katika Bara la Afrika imekuwa ikikuwa kutokana na mizigo mingi inayosafirishwa duniani inatoka na kuja Afrika.
Bw. Migire ameyasema hayo leo Februari 27, 2023 wakati wa Mkutano wa Taasisi inayojihusisha na masuala ya usafirishaji wa majini (ISCOS), uliofanyika katika hoteli ya Four Points jijini Dar es salaam.
“Sisi kama Waafrika tuna kila sababu ya kuhakikisha tunakuwa na watu wanamiliki vyombo vya usafiri majini”.
Aidha amesema kuna changamoto ya ukosefu wa vyombo vya kujifunzia kwa upande wa wanafunzi wanaosoma Chuo cha Bahari (DMI) pindi wanapomaliza mafunzo hayo ya ubaharia.
“Tunahitaji kuwa na vyombo vyetu lakini pia tunahitaji vyombo hivi kwa ajili ya kufanya biashara kwa sababu Afrika sasa hivi inafunguliwa kibiashara” Amesema Bw. Migire.
” Sisi kwenye eneo hili la Afrika Mashariki na ISCOS member state tunakila sababu ya kuhakikisha kwamba tunatumia hiyo fursa ya kushiriki kwenye hiyo biashara ya Afrika, Tunavyofunguliana nchi za Afrika haina maana kwamba turuhusu mabara mengine yaje tafanye biashara Afrika ,ni sisi nchi za Afrika tunatakiwa kuhakikisha tunatumia hiyo fursa” Ameongeza Bw. Migire.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa ISCOS, Daniel Kiange amesema kwa sasa Wakati umefika wa Afrika kuweza kuwa na vyombo vya usafirishaji ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kwenda ughaibuni.
“Tuweze kuwa na meli zetu ambazo zinaweza kubeba mizigo kwenda China,South Africa na kule kwingine ili hiyo pesa iweze kubaki katika Kanda yetu, na pia tuweze kutengeneza nafasi za kazi kwa ajili ya vijana wetu” Amesema Kiange.
Naye Katibu Mtendaji wa chama cha wamiliki wa meli barani Afrika (African Shipowners Association), Bi.Funmi Folorunso amesema kufuatia mkutano huo wanatarajia Nchi Wananchama wa ISCOS watakuja na sera ya umiliki wa meli katika kusaidia sekta ya usafirishaji.
Godwin Isdore kutoka Songoro Marine ni mmoja wa wadau walioshiriki mkutano huo amesema ni kushiriki katika mkutano huo ni ya kuongeza maarifa pamoja na kujenga uhusiano na wadau kutoka nchi wanachama wa Iscos wakiwemo kutoka Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
“Tukiangalia katika Afrika , moja kati ya biashara kubwa inayofanyika ni Shipping na kama unavyoona wadau wameamka na wanasema ni muda sasa wa kumiliki meli” Amesema Godwin.
Intergovernmental Standing Committee on Shipping (ISCOS) ni taasisi inayojihusisha na masuala ya usafirishaji wa majini ambayo kwa sasa inazijumuisha nchi za TANZANIA, KENYA, UGANDA ZAMBIA na DRC.

More Posts

News • 04 Apr, 2024
ASA-NG Courtesy Visit to the Lagos State Ministry of Transpo…

ASA-NG Courtesy Visit to the Lagos State Ministry of Transportation on 3rd April 2024

News • 14 Mar, 2024
ASA delegation visits EUROPEAN UNION office in Cote D’…

On 13th March 2024, the Secretary General, African Shipowners Association, led an ASA delegation to the EUROPEAN UNION office in...

Translate »